# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # mataifa Hii inamaanisha watu wa mataifa. "watu wa mataifa yote" # yatetemeke kutetemeka kwa hofu # Ameketi amesimikwa juu ya makerubi Mwandishi wa zaburi anazungumza kana kwamba kiti cha enzi ambacho yahwe hukaa ni juu ya makerubi kwenye mfuniko wa amri za sanduku la agano hekaluni. # inatetemeka inatikisika # Yahwe ni mkuu Sayuni; ameinuliwa juu ya mataifa yote "Sio tu kwamba Yahwe ni mkuu sayuni, ametukuka juu ya mataifa yote" au "Sio tu kwamba Yahwe anatawala Sayuni, anatawala juu ya mataifa yote" # ameinuliwa juu ya mataifa yote Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "watu katika mataifa yote wanamtukuza" au "watu katika mataifa yote wanamsifu sana" # Acha walisifu jina lako kuu na la ajabu Hapa mwandishi anahama kutoka kumzungumzia Mungu na kuzungumza na Mungu. Ingawa baada ya msemo huu, anarudi tena kumzungumzia Mungu.