sw_tn/psa/085/008.md

16 lines
640 B
Markdown

# atafanya amani na watu wake
"atakuwa na mahusiano ya amani na watu wake" au "ataleta amani kwa watu wake"
# Bali wasirudie tena njia zao za upumbavu
Mtu anayebadili tabia yake anazungumziwa kana kwamba alikuwa akigeukia kimwili upande mwingine. "Bali hawatakiwa kuanza kufanya mambo ya upambavu tena"
# Hakika wokovu wake uko karibu na wale
Mungu kuwa tayari kumwokoa mtu inazungumziwa kana kwamba wokovu ni kitu ambacho Mungu ameweka karibu na mtu. "Hakika Mungu yuko tayari kuwaokoa wale"
# kisha utukufu utabaki katika nchi yetu
Hapa "utukufu" unawakilisha uwepo wa Mungu. "kisha uwepo wake wa utukufu utabaki katika nchi yetu"