# atafanya amani na watu wake "atakuwa na mahusiano ya amani na watu wake" au "ataleta amani kwa watu wake" # Bali wasirudie tena njia zao za upumbavu Mtu anayebadili tabia yake anazungumziwa kana kwamba alikuwa akigeukia kimwili upande mwingine. "Bali hawatakiwa kuanza kufanya mambo ya upambavu tena" # Hakika wokovu wake uko karibu na wale Mungu kuwa tayari kumwokoa mtu inazungumziwa kana kwamba wokovu ni kitu ambacho Mungu ameweka karibu na mtu. "Hakika Mungu yuko tayari kuwaokoa wale" # kisha utukufu utabaki katika nchi yetu Hapa "utukufu" unawakilisha uwepo wa Mungu. "kisha uwepo wake wa utukufu utabaki katika nchi yetu"