sw_tn/psa/044/012.md

32 lines
963 B
Markdown

# Unawauza watu wako bure
Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwaruhusu adui wa Israeli kuwashinda kana kwamba alikuwa akiwauza watu wa Israeli kwa adui zao lakini hahitaji malipo kutoka kwa adui zao.
# Unatufanya kuwa lawama kwa jirani zetu, kudhihakiwa na kukejeliwa na wale waliotuzunguka
Misemo hii miwili ina usambamba ikisisitiza jinsi watu wanaoishi miongoni mwao wanavyowakejeli.
# Unatufanya kuwa lawama kwa jirani zetu
"Unatufanya kuwa kitu ambacho jirani zetu wanakemea"
# kudhihakiwa na kukejeliwa na wale waliotuzunguka
"wale waliotuzunguka wanatudhihaki na kutukejeli"
# fedheha miongoni ... kutikisa kichwa
Misemo hii miwili ina usambamba ikisisitiza jinsi watu wanavyowakejeli kwa nguvu.
# Umetufanya fedheha miongoni mwa mataifa
Unayafanya mataifa yaliyo tuzunguka kutufedhehesha"
# kutikisa kichwa miongoni mwa watu
"jambo ambalo watu hutikisa vichwa"
# kutikisa kichwa
Hiki ni kitendeo ambacho watu walitumia kuonesha dharau wengine.