# Unawauza watu wako bure Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwaruhusu adui wa Israeli kuwashinda kana kwamba alikuwa akiwauza watu wa Israeli kwa adui zao lakini hahitaji malipo kutoka kwa adui zao. # Unatufanya kuwa lawama kwa jirani zetu, kudhihakiwa na kukejeliwa na wale waliotuzunguka Misemo hii miwili ina usambamba ikisisitiza jinsi watu wanaoishi miongoni mwao wanavyowakejeli. # Unatufanya kuwa lawama kwa jirani zetu "Unatufanya kuwa kitu ambacho jirani zetu wanakemea" # kudhihakiwa na kukejeliwa na wale waliotuzunguka "wale waliotuzunguka wanatudhihaki na kutukejeli" # fedheha miongoni ... kutikisa kichwa Misemo hii miwili ina usambamba ikisisitiza jinsi watu wanavyowakejeli kwa nguvu. # Umetufanya fedheha miongoni mwa mataifa Unayafanya mataifa yaliyo tuzunguka kutufedhehesha" # kutikisa kichwa miongoni mwa watu "jambo ambalo watu hutikisa vichwa" # kutikisa kichwa Hiki ni kitendeo ambacho watu walitumia kuonesha dharau wengine.