sw_tn/psa/036/001.md

36 lines
918 B
Markdown

# Taarifa ya Jumla:
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Kwa mwanamuziki mkuu
"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"
# Zaburi ya Daudi mtumishi wa Yahwe
Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi.
# Dhambi inazungumza kama mwaguzi
Dhambi inaelezwa kana kwamba ni nabii wa uongo. "Dhambi ni kama nabii wa uongo anayezungumza"
# katika moyo wa mtu mwovu
Hapa "moyo" inamaanisha hali ya ndani wa mtu. "hali ya ndani ya mtu mwovu"
# mtu mwovu
Hii haimaanishi mtu bayana, lakini kwa watu waovu kwa ujumla. "watu waovu"
# katika macho yake
Hapa "macho" yanamaanisha mtu mwovu. "ndani yake"
# anajifariji, akifikiri
"anapendelea kuamini" au "anataka kufikiri"
# dhambi yake haitagunduliwa na kuchukiwa
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu hatagundua na kuchukia dhambi yake"