# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # Zaburi ya Daudi mtumishi wa Yahwe Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # Dhambi inazungumza kama mwaguzi Dhambi inaelezwa kana kwamba ni nabii wa uongo. "Dhambi ni kama nabii wa uongo anayezungumza" # katika moyo wa mtu mwovu Hapa "moyo" inamaanisha hali ya ndani wa mtu. "hali ya ndani ya mtu mwovu" # mtu mwovu Hii haimaanishi mtu bayana, lakini kwa watu waovu kwa ujumla. "watu waovu" # katika macho yake Hapa "macho" yanamaanisha mtu mwovu. "ndani yake" # anajifariji, akifikiri "anapendelea kuamini" au "anataka kufikiri" # dhambi yake haitagunduliwa na kuchukiwa Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Mungu hatagundua na kuchukia dhambi yake"