sw_tn/psa/035/004.md

40 lines
1.0 KiB
Markdown

# Na wale wanaotafuta maisha yangu waaibike na kunyimwa heshima
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na Yahwe awaaibishe na kuwanyima heshima wale wanaotafuta maisha yangu"
# Na
"Natamani kwamba"
# wanaotafuta maisha yangu
Hapa "maisha yangu" inamaana wanatamani kumuua mwandishi. "wanaojaribu kuniua"
# Na wale wanaopanga kunidhuru wageuzwe na washangazwe
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Na Yahwe awageuze na kuwashangaza wale wanaopanga kunidhuru"
# wageuzwe
"wageuzwe" ni sitiari ya kushindwa kutimiza lengo lao. "kushindwa kufanikiwa"
# washangazwe
"wachanganyikiwe" au "kuwafadhaisha"
# kama makapi mbele ya upepo
Adui wa mwandishi wanazungumziwa kana kwamba ni nyasi ambayo inapulizwa kwa urahisi. "kupulizwa na upepo kama makapi"
# njia yao
Hapa "njia yao" inamaanisha maisha yao. "maisha yao"
# giza na utelezi
Hii inamaanisha njia iliyojificha na hatari. "imejificha na imejaa hatari"
# anawafukuza
Hii inamaanisha malaika wa Yahwe kuwa kinyume na adui wa mwandishi. "anaenda kinyume nao" au "anawapinga"