sw_tn/pro/01/20.md

32 lines
1017 B
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Katika 1:20-1:33 Hekima inaongelewa mithili ya mwanamke anayeongea na watu.
# Hekima analia kwa sauti
"Hekima ni kama mwanamke ambaye hulia kwa sauti kuu"
# hupaza sauti yake
Hii ni nahau "Huongea kwa sauti kuu"
# katika viwanja
sehemu ambapo huweza kuwa na watu wengi. "kwenye soko" au "katika viunga vya mji"
# kwenye kelele kuu za mitaa
sehemu ambapo mitaa yenye shughuli nyingi imeunganika au juu ya ukuta ambapo watu walioko kwenye kelele za mitaa wanaweza kuona na kusikia hekima ikiongea.
# Hata lini, ninyi watu wajinga, mtapenda kuwa wajinga?
Hekima anatumia swali hili kuwakemea wasio na hekima. "Ninyi ambao ni wajinga lazima mkome kupenda kuwa wajinga"
# wajinga
"bila uzoefu, isiyo komavu/uchanga"
# Hata lini, ninyi wenye dhihaka, mtapenda dhihaka, na hata lini, ninyi wapumbavu, mtachukia maarifa?
Hekima anatumia swali hili kuwakema wenye dhihaka na wapumbavu. " Ninyi ambao hudhihaki lazima muache kupenda dhihaki, na ninyi wapumbavu lazima muache kuchukia maarifa"