sw_tn/pro/01/20.md

1017 B

Maelezo ya Jumla

Katika 1:20-1:33 Hekima inaongelewa mithili ya mwanamke anayeongea na watu.

Hekima analia kwa sauti

"Hekima ni kama mwanamke ambaye hulia kwa sauti kuu"

hupaza sauti yake

Hii ni nahau "Huongea kwa sauti kuu"

katika viwanja

sehemu ambapo huweza kuwa na watu wengi. "kwenye soko" au "katika viunga vya mji"

kwenye kelele kuu za mitaa

sehemu ambapo mitaa yenye shughuli nyingi imeunganika au juu ya ukuta ambapo watu walioko kwenye kelele za mitaa wanaweza kuona na kusikia hekima ikiongea.

Hata lini, ninyi watu wajinga, mtapenda kuwa wajinga?

Hekima anatumia swali hili kuwakemea wasio na hekima. "Ninyi ambao ni wajinga lazima mkome kupenda kuwa wajinga"

wajinga

"bila uzoefu, isiyo komavu/uchanga"

Hata lini, ninyi wenye dhihaka, mtapenda dhihaka, na hata lini, ninyi wapumbavu, mtachukia maarifa?

Hekima anatumia swali hili kuwakema wenye dhihaka na wapumbavu. " Ninyi ambao hudhihaki lazima muache kupenda dhihaki, na ninyi wapumbavu lazima muache kuchukia maarifa"