# Maelezo ya Jumla Katika 1:20-1:33 Hekima inaongelewa mithili ya mwanamke anayeongea na watu. # Hekima analia kwa sauti "Hekima ni kama mwanamke ambaye hulia kwa sauti kuu" # hupaza sauti yake Hii ni nahau "Huongea kwa sauti kuu" # katika viwanja sehemu ambapo huweza kuwa na watu wengi. "kwenye soko" au "katika viunga vya mji" # kwenye kelele kuu za mitaa sehemu ambapo mitaa yenye shughuli nyingi imeunganika au juu ya ukuta ambapo watu walioko kwenye kelele za mitaa wanaweza kuona na kusikia hekima ikiongea. # Hata lini, ninyi watu wajinga, mtapenda kuwa wajinga? Hekima anatumia swali hili kuwakemea wasio na hekima. "Ninyi ambao ni wajinga lazima mkome kupenda kuwa wajinga" # wajinga "bila uzoefu, isiyo komavu/uchanga" # Hata lini, ninyi wenye dhihaka, mtapenda dhihaka, na hata lini, ninyi wapumbavu, mtachukia maarifa? Hekima anatumia swali hili kuwakema wenye dhihaka na wapumbavu. " Ninyi ambao hudhihaki lazima muache kupenda dhihaki, na ninyi wapumbavu lazima muache kuchukia maarifa"