sw_tn/pro/01/12.md

32 lines
1023 B
Markdown

# Maelezo ya Jumla
Mstari 12-14 ni mwisho wa kauli ya kihisia ya waovu ambao wanajaribu kuwashawishi wengine kufanya dhambi.
# Tuwameze wangali hai, kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya
wenye dhambi wanaongea juu ya kuwaua watu wasio na hatia kama kuzimu ambavyo hupeleka chini kwa wafu watu wenye afya.
# Tuwameze..., kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya
kaburi linafananishwa kama mtu ambaye huwameza wanadamu na kuwapeleka chini katika sehemu ya wafu.
# kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya
waovu wanatarajia kuwaangamiza mateka wao kwa jinsi ile ile ambayo kuzimu(sehemu ya wafu) inavyowachukua hata watu wenye afya.
# tuwafanye kama wale ambao huanguka kwenye shimo
"shimo" ni neno jingine lenye maana ya kuzimu au sehemu ambayo wafu huishi.
# Tupa kura yako pamoja nasi
Hii ni nahau "jiunge nasi"
# Sisi kwa pamoja tutakuwa na mkoba mmoja
"Mkoba" hapa unawakilisha kila kitu wanachoiba. "Sisi tutagawana kwa usawa kila kitu ambacho tumeiba"
# mkoba
begi kwa ajili ya kubebea fadha