# Maelezo ya Jumla Mstari 12-14 ni mwisho wa kauli ya kihisia ya waovu ambao wanajaribu kuwashawishi wengine kufanya dhambi. # Tuwameze wangali hai, kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya wenye dhambi wanaongea juu ya kuwaua watu wasio na hatia kama kuzimu ambavyo hupeleka chini kwa wafu watu wenye afya. # Tuwameze..., kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya kaburi linafananishwa kama mtu ambaye huwameza wanadamu na kuwapeleka chini katika sehemu ya wafu. # kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya waovu wanatarajia kuwaangamiza mateka wao kwa jinsi ile ile ambayo kuzimu(sehemu ya wafu) inavyowachukua hata watu wenye afya. # tuwafanye kama wale ambao huanguka kwenye shimo "shimo" ni neno jingine lenye maana ya kuzimu au sehemu ambayo wafu huishi. # Tupa kura yako pamoja nasi Hii ni nahau "jiunge nasi" # Sisi kwa pamoja tutakuwa na mkoba mmoja "Mkoba" hapa unawakilisha kila kitu wanachoiba. "Sisi tutagawana kwa usawa kila kitu ambacho tumeiba" # mkoba begi kwa ajili ya kubebea fadha