sw_tn/pro/01/12.md

1023 B

Maelezo ya Jumla

Mstari 12-14 ni mwisho wa kauli ya kihisia ya waovu ambao wanajaribu kuwashawishi wengine kufanya dhambi.

Tuwameze wangali hai, kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya

wenye dhambi wanaongea juu ya kuwaua watu wasio na hatia kama kuzimu ambavyo hupeleka chini kwa wafu watu wenye afya.

Tuwameze..., kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya

kaburi linafananishwa kama mtu ambaye huwameza wanadamu na kuwapeleka chini katika sehemu ya wafu.

kama kuzimu inavyowachukua wale wenye afya

waovu wanatarajia kuwaangamiza mateka wao kwa jinsi ile ile ambayo kuzimu(sehemu ya wafu) inavyowachukua hata watu wenye afya.

tuwafanye kama wale ambao huanguka kwenye shimo

"shimo" ni neno jingine lenye maana ya kuzimu au sehemu ambayo wafu huishi.

Tupa kura yako pamoja nasi

Hii ni nahau "jiunge nasi"

Sisi kwa pamoja tutakuwa na mkoba mmoja

"Mkoba" hapa unawakilisha kila kitu wanachoiba. "Sisi tutagawana kwa usawa kila kitu ambacho tumeiba"

mkoba

begi kwa ajili ya kubebea fadha