sw_tn/num/11/11.md

24 lines
909 B
Markdown

# Taarifa kwa ujumla
Musa anamlalamikia BWANA akitumia maswali mengi yasitotaka majibu.
# Kwa nini umemtendea mtumishi wako vibaya namna? kwa nini hujapendezwa na mimi?
"usinitendee mimi, mtumishi wako, vibaya namna hiyo." au "usiwe na hasira dhidi yangu."
# Umenifanya kubeba mizigo ya hawa watu
"umenifanya niajibike kwa ajili ya hawa watu"
# Je, mimi ndiye niliyewatungia mimba hawa watu? Mimi ndiye niliyewazaa kiasi kwamba unaniambia?
"Mimi si baba wa hawa watu. Kwa hiyo si sahihi kuniambia mimi."
# wabebe kwa ukaribu vifufani mwako kama baba abebavyo mtoto wake
Maana yake ni kwamba Musa analazimika kuajibika kwa watu ambao hawawezi kujilinda wenyewe, kama vile mzazi alindavyo kichanga.
# Je, nitawabeba mpaka kwenye nchi ... mababu zao kuwapa?
""Usinitegeme mimi kuwabeba... mpaka kwenye uliyowaahidi mababu zao kuwapa" au "siwezi kuwabeba... mpaka kwenye nchi uliyowaahidi mababu zao."