# Taarifa kwa ujumla Musa anamlalamikia BWANA akitumia maswali mengi yasitotaka majibu. # Kwa nini umemtendea mtumishi wako vibaya namna? kwa nini hujapendezwa na mimi? "usinitendee mimi, mtumishi wako, vibaya namna hiyo." au "usiwe na hasira dhidi yangu." # Umenifanya kubeba mizigo ya hawa watu "umenifanya niajibike kwa ajili ya hawa watu" # Je, mimi ndiye niliyewatungia mimba hawa watu? Mimi ndiye niliyewazaa kiasi kwamba unaniambia? "Mimi si baba wa hawa watu. Kwa hiyo si sahihi kuniambia mimi." # wabebe kwa ukaribu vifufani mwako kama baba abebavyo mtoto wake Maana yake ni kwamba Musa analazimika kuajibika kwa watu ambao hawawezi kujilinda wenyewe, kama vile mzazi alindavyo kichanga. # Je, nitawabeba mpaka kwenye nchi ... mababu zao kuwapa? ""Usinitegeme mimi kuwabeba... mpaka kwenye uliyowaahidi mababu zao kuwapa" au "siwezi kuwabeba... mpaka kwenye nchi uliyowaahidi mababu zao."