sw_tn/nam/02/01.md

36 lines
949 B
Markdown

# Maelezo ya jumla:
Nahumu anaelezea uharibifu wa Ninawi katika shairi.
# Yule ambaye atakuvunja vipande vipande
Ni namna ya picha ya mtu anayevunja chungu. TN: " Atakuharibu"
# Yule ambaye atakuvunja
Mtu ambaye ni "Yule" hajawekwa wazi, kwa hiyo tafsiri inatumia kauli jumuishi: "mtu ambaye atakuvunja vipande vipande."
# Linda kuta za mji, linda barabara, jitieni nguvu ninyi wenyewe, yakusanyeni majeshi yenu.
kujitayarisha kwa ajili vita
# Linda kuta za mji
"Panga walinzi kwenye kuta kwa ajili ya kukinga"
# Maana Yahwe anarejesha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli
Hii inamaana kuwa Yahwe atamfanya Yakobo na Israeli kuwa wakuu, na watu watawapenda tena.
# wateka nyara
watu wanaoiba vitu kwa nguvu, mara nyingi katika vita
# waliwaharibu
waliangamiza kila kitu.
# kuharibu matawi ya zabibu zao
hapa taifa linaongelewa kana kwamba ni mzabibu uliolimwa. TN: " na kuling'oa taifa lenu kana kwamba ni shamba la mzabibu"