sw_tn/nam/02/01.md

949 B

Maelezo ya jumla:

Nahumu anaelezea uharibifu wa Ninawi katika shairi.

Yule ambaye atakuvunja vipande vipande

Ni namna ya picha ya mtu anayevunja chungu. TN: " Atakuharibu"

Yule ambaye atakuvunja

Mtu ambaye ni "Yule" hajawekwa wazi, kwa hiyo tafsiri inatumia kauli jumuishi: "mtu ambaye atakuvunja vipande vipande."

Linda kuta za mji, linda barabara, jitieni nguvu ninyi wenyewe, yakusanyeni majeshi yenu.

kujitayarisha kwa ajili vita

Linda kuta za mji

"Panga walinzi kwenye kuta kwa ajili ya kukinga"

Maana Yahwe anarejesha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli

Hii inamaana kuwa Yahwe atamfanya Yakobo na Israeli kuwa wakuu, na watu watawapenda tena.

wateka nyara

watu wanaoiba vitu kwa nguvu, mara nyingi katika vita

waliwaharibu

waliangamiza kila kitu.

kuharibu matawi ya zabibu zao

hapa taifa linaongelewa kana kwamba ni mzabibu uliolimwa. TN: " na kuling'oa taifa lenu kana kwamba ni shamba la mzabibu"