# Maelezo ya jumla: Nahumu anaelezea uharibifu wa Ninawi katika shairi. # Yule ambaye atakuvunja vipande vipande Ni namna ya picha ya mtu anayevunja chungu. TN: " Atakuharibu" # Yule ambaye atakuvunja Mtu ambaye ni "Yule" hajawekwa wazi, kwa hiyo tafsiri inatumia kauli jumuishi: "mtu ambaye atakuvunja vipande vipande." # Linda kuta za mji, linda barabara, jitieni nguvu ninyi wenyewe, yakusanyeni majeshi yenu. kujitayarisha kwa ajili vita # Linda kuta za mji "Panga walinzi kwenye kuta kwa ajili ya kukinga" # Maana Yahwe anarejesha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli Hii inamaana kuwa Yahwe atamfanya Yakobo na Israeli kuwa wakuu, na watu watawapenda tena. # wateka nyara watu wanaoiba vitu kwa nguvu, mara nyingi katika vita # waliwaharibu waliangamiza kila kitu. # kuharibu matawi ya zabibu zao hapa taifa linaongelewa kana kwamba ni mzabibu uliolimwa. TN: " na kuling'oa taifa lenu kana kwamba ni shamba la mzabibu"