sw_tn/mic/04/02.md

24 lines
925 B
Markdown

# njooni tuupande mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo
Vyote mlima na nyumba ni kumbukumbu kwa hekalu la Yerusalemu.
# Atatufundisha njia zake, na tutaenenda katika njia zake
Hapa "njia zake" na "njia zake" zinarejea kwa kile ambacho Mungu ataka watu wakifanye. Pia, "kuenenda" maana yake watatii kile asemacho.
# Kwa kuwa kutoka Sayuni sheria itatoka, na neno la Yahwe kutoka Yerusalemu
Hapa maneno "sheria" na "neno" yanazungumzia jambo moja. Mataifa ya dunia watasikiliza sheria ya Mungu katika Yerusalemu.
# plau
Plau ni kengee ambayo watu hutumia kulimia kwenye udongo ili wapande mbegu.
# Watazipiga panga zao kwenye plau na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea
Virai hivi vyote vinamaanisha kwamba watarudisha silaha zao za vita kwenye vifaa watakavyovitumia kuandalia chakula.
# miundu ya kupogolea
Mundu wa kupogolea unatumika kukatia matawi au au visiki kutoka kwenye mmea kuufanya uzae vema.