# njooni tuupande mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo Vyote mlima na nyumba ni kumbukumbu kwa hekalu la Yerusalemu. # Atatufundisha njia zake, na tutaenenda katika njia zake Hapa "njia zake" na "njia zake" zinarejea kwa kile ambacho Mungu ataka watu wakifanye. Pia, "kuenenda" maana yake watatii kile asemacho. # Kwa kuwa kutoka Sayuni sheria itatoka, na neno la Yahwe kutoka Yerusalemu Hapa maneno "sheria" na "neno" yanazungumzia jambo moja. Mataifa ya dunia watasikiliza sheria ya Mungu katika Yerusalemu. # plau Plau ni kengee ambayo watu hutumia kulimia kwenye udongo ili wapande mbegu. # Watazipiga panga zao kwenye plau na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea Virai hivi vyote vinamaanisha kwamba watarudisha silaha zao za vita kwenye vifaa watakavyovitumia kuandalia chakula. # miundu ya kupogolea Mundu wa kupogolea unatumika kukatia matawi au au visiki kutoka kwenye mmea kuufanya uzae vema.