forked from WA-Catalog/sw_tn
925 B
925 B
njooni tuupande mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo
Vyote mlima na nyumba ni kumbukumbu kwa hekalu la Yerusalemu.
Atatufundisha njia zake, na tutaenenda katika njia zake
Hapa "njia zake" na "njia zake" zinarejea kwa kile ambacho Mungu ataka watu wakifanye. Pia, "kuenenda" maana yake watatii kile asemacho.
Kwa kuwa kutoka Sayuni sheria itatoka, na neno la Yahwe kutoka Yerusalemu
Hapa maneno "sheria" na "neno" yanazungumzia jambo moja. Mataifa ya dunia watasikiliza sheria ya Mungu katika Yerusalemu.
plau
Plau ni kengee ambayo watu hutumia kulimia kwenye udongo ili wapande mbegu.
Watazipiga panga zao kwenye plau na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea
Virai hivi vyote vinamaanisha kwamba watarudisha silaha zao za vita kwenye vifaa watakavyovitumia kuandalia chakula.
miundu ya kupogolea
Mundu wa kupogolea unatumika kukatia matawi au au visiki kutoka kwenye mmea kuufanya uzae vema.