sw_tn/mat/24/intro.md

1.3 KiB

Mathayo 24 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Katika sura hii, Yesu anaanza kutabiri kuhusu wakati ujao kutoka wakati huo hadi atakaporudi kama mfalme wa ulimwengu. (Angalia: rc://*/tw/dict/bible/kt/prophet)

Dhana maalum katika sura hii

"Mwisho wa ulimwengu"

Katika sura hii, Yesu anatoa jibu kwa wanafunzi wake wakati wanauliza jinsi watakavyojua wakati atakapokuja tena. (See: rc://*/ta/man/translate/writing-apocalypticwriting)

Mfano wa Nuhu

Katika wakati wa Nuhu, Mungu alituma gharika kuu kuwaadhibu watu kwa dhambi zao. Aliwaonya mara nyingi kuhusu kuja kwa mafuriko hayo, lakini kwa hakika yalianza ghafla. Katika sura hii, Yesu analinganisha mafuriko hayo na siku za mwisho. (Angalia: rc://*/tw/dict/bible/kt/sin)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Ruhusu"

ULB hutumia neno hili kuanzisha amri kadhaa za Yesu, kama "wacha wale walio Yudea wakimbilie milimani" (24:16), "yule aliye juu ya nyumba asije akashuka kuchukua chochote kutoka kwa nyumba yake "(24:17), na" aliye mashambani asirudi kuchukua nguo yake "(24:18). Kuna njia nyingi za kuunda amri. Watafsiri wanapaswa kuchagua njia za asili zaidi katika lugha zao wenyewe.

<< | >>