sw_tn/mat/21/intro.md

24 lines
870 B
Markdown

# Mathayo 21 Maelezo ya Jumla
## Muundo na upangiliaji
Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka kando kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari yote ya 21:5,16 na 42, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.
## Dhana maalum katika sura hii
### Hosana
Hili ndilo neno ambalo watu walisema wakipiga kelele walipomkaribisha Yesu huko Yerusalemu. Ilikuwa ni tamko la sifa, ingawa pia ilikuwa neno la Kiebrania linalomaanisha, "Tuokoe!"
## Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii
### "Ufalme wa Mungu utaondolewa kutoka kwenu"
Wasomi wametofautiana kuhusu maana ya maneno haya. Swali muhimu ni hili: Je, tukio hili itakuwa la kudumu au la muda? Ikiwezekana, uziache wezekano zote mbili kuwa wazi katika tafsiri yako.
## Links:
* __[Matthew 21:01 Notes](./01.md)__
__[<<](../20/intro.md) | [>>](../22/intro.md)__