# Mathayo 21 Maelezo ya Jumla ## Muundo na upangiliaji Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka kando kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari yote ya 21:5,16 na 42, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale. ## Dhana maalum katika sura hii ### Hosana Hili ndilo neno ambalo watu walisema wakipiga kelele walipomkaribisha Yesu huko Yerusalemu. Ilikuwa ni tamko la sifa, ingawa pia ilikuwa neno la Kiebrania linalomaanisha, "Tuokoe!" ## Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii ### "Ufalme wa Mungu utaondolewa kutoka kwenu" Wasomi wametofautiana kuhusu maana ya maneno haya. Swali muhimu ni hili: Je, tukio hili itakuwa la kudumu au la muda? Ikiwezekana, uziache wezekano zote mbili kuwa wazi katika tafsiri yako. ## Links: * __[Matthew 21:01 Notes](./01.md)__ __[<<](../20/intro.md) | [>>](../22/intro.md)__