sw_tn/mat/12/intro.md

1.4 KiB

Mathayo12 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea huingiza kidogo mistari ya nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari yote ya 12: 18-21, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Sabato

Kutii Sabato ni sehemu muhimu katika sura hii. Hata hivyo, Yesu anafafanua kati ya kufuata Sabato jinsi Mungu alivyoamuru na kufuata sheria ambazo Mafarisayo waliziunda kuhusu Sabato. (Angalia: rc://*/tw/dict/bible/kt/sabbath)

"Kukufuru Roho"

Kuna utata mkubwa juu ya kutambua vizuri dhambi hii maalum. Hata hivyo, inaonekana kuwa inahusisha kumtukana Roho Mtakatifu na kazi yake. Kwa kuwa sehemu ya kazi yake ni kuwashawishi watu kuwa wao ni wenye dhambi na kwamba wanahitaji msamaha wa Mungu, yeyote ambaye alikejeli ukweli huu hangetaka kuja kwake Mungu kwa toba. Kwa sababu hii, hangeweza kusamehewa. (Angalia: rc://*/tw/dict/bible/kt/sin)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kaka na Dada

Sura hii inaanzisha dhana ya kaka na dada "wa kiroho". Maandiko hutumia maneno haya kwa kutaja uhusiano kati ya Waisraeli. Hapa, wale wanaomfuata Yesu sasa wanajulikana kama kaka na dada. (Angalia: [[rc:///tw/dict/bible/kt/spirit]] na [[rc:///tw/dict/bible/kt/brother]])

<< | >>