sw_tn/mat/10/intro.md

1.7 KiB

Mathayo 10 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Kutumwa kwa wanafunzi kumi na wawili

Sehemu kubwa ya sura hii inazungumza juu ya Yesu kuwatuma wanafunzi kumi na wawili kutoa ujumbe wake kuhusu ufalme wa mbinguni. Walipaswa kufanya huduma yao kwa inchi ya Israeli pekee na wasije wakashiriki habari hii kwa wasio Wayahudi. Maagizo ya Yesu humpa msomaji hisia kwamba hawakupaswa kupoteza wakati wowote. Sauti yake iliashiria kuwa alitaka waharakishe.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Wanafunzi kumi na wawili

Yafuatayo ni orodha ya wanafunzi kumi na wawili: Katika Mathayo: Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo, Yohana mwana wa Zebedayo, Filipo, Bartholomayo, Tomasi, Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mzeloti na Yuda Iskarioti.

Katika Marko: Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana mwana wa Zebedayo (ambaye aliwaita Boanerge, yaani, wana wa ngurumo), Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mzeloti, na Yuda Iskarioti.

Katika Luka: Simoni (Petro), Andrea, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni (aitwaye Mzeloti, Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda "Iskarioti.

Inawezekana kuwa Thadayo na Yuda, mwana wa Yakobo, ni majina mawili ya mtu mmoja.

"Ufalme wa mbinguni umekaribia"

Maneno haya yana umuhimu mkubwa wa kitheolojia. Wataalam wanajadili ikiwa "ufalme wa mbinguni" ulikuwepo wakati huu au bado unakuja. Tafsiri za Kiingereza mara nyingi hutumia maneno "karibu," lakini hii inaweza kusababisha changamoto katika kutafsiri. Matoleo mengine hutumia maneno "inakaribia" na "yamekaribia."

<< | >>