sw_tn/luk/24/30.md

1015 B

Ilitokea

Neno hili limetumika hapa kuashiria tukio muhimu katika simulizi.

mkate

Hii inazungumzia juu ya mkate unaotengenezwa bila hamila. Haimaanishi chakula kwa ujumla.

akaubariki

"akashukuru kwa ajili ya huo mkate" au "Akamshukuru Mungu kwa ajili ya mkate"

Kisha macho yao yakafunguliwa

Tafsiri mbadala: "kisha wakaelewa" au "kisha wakatambua"

akatoweka ghafla mbele ya macho yao

Hii inamaanisha kwamba ghafula hakuwa tena pale. Haimaanishi kwamba akawa haonekani kwa macho.

Hivi mioyo yetu haikuwaka... maandiko?

Wanatumia swali kuweka msisitizo namna walivyo shangazwa juu ya kukutana kwao na Yesu. Tafsiri mbadala: "Mioyo yetu ilikuwa ikiwaka ndani yetu...maandiko."

ikiwaka ndani yetu

Hii ni lugha ya picha inayoelezea hisia kali walizokuwa nazo walipokuwa wakiongea na Yesu. Tafsiri mbadala: "Tulikuwa na hisia kali alipokuwa akiongea na sisi."

wakati alipotufungulia maandiko

Yesu hakufungua kitabu au gombo la chuo. Tafsiri mbadala: "wakati alipokuwa akituelezea maandiko.