# Ilitokea Neno hili limetumika hapa kuashiria tukio muhimu katika simulizi. # mkate Hii inazungumzia juu ya mkate unaotengenezwa bila hamila. Haimaanishi chakula kwa ujumla. # akaubariki "akashukuru kwa ajili ya huo mkate" au "Akamshukuru Mungu kwa ajili ya mkate" # Kisha macho yao yakafunguliwa Tafsiri mbadala: "kisha wakaelewa" au "kisha wakatambua" # akatoweka ghafla mbele ya macho yao Hii inamaanisha kwamba ghafula hakuwa tena pale. Haimaanishi kwamba akawa haonekani kwa macho. # Hivi mioyo yetu haikuwaka... maandiko? Wanatumia swali kuweka msisitizo namna walivyo shangazwa juu ya kukutana kwao na Yesu. Tafsiri mbadala: "Mioyo yetu ilikuwa ikiwaka ndani yetu...maandiko." # ikiwaka ndani yetu Hii ni lugha ya picha inayoelezea hisia kali walizokuwa nazo walipokuwa wakiongea na Yesu. Tafsiri mbadala: "Tulikuwa na hisia kali alipokuwa akiongea na sisi." # wakati alipotufungulia maandiko Yesu hakufungua kitabu au gombo la chuo. Tafsiri mbadala: "wakati alipokuwa akituelezea maandiko.