sw_tn/luk/21/34.md

32 lines
959 B
Markdown

# ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa
Tafsiri mbadala: "ili msije mkawa mmetingwa na"
# ufisadi
"tamaa isiyoweza kuzuiwa" au " kujiweka kwenye kutamani na kutumia vitu ambavyo vinakufanya ujisikie vizuri." Tafsiri mbadala: "Anasa nyingi."
# mahangaiko ya maisha haya
"kujitaabisha au kujihangaisha sana kuhusu maisha haya"
# kwa sababu siku ile itawajia ghafula
Wengine wangependa kuongeza habari elekezi: "Kwamba kama hamtakuwa waangalifu ile siku itawajia ghafula." Ujio wa siku hiyo utaonekana kuwa wa ghafula na wakutotarajiwa kwa wale ambao hawako na hawaisubiri.
# ile siku
Tafsiri mbadala: "siku ambayo Mwana wa Adamu atakuja"
# ghafula kama mtego
Tafsiri mbadala: "wakati ambapo hamuitarajii, kama mtego unapofunga ghafula kwa mnyama"
# itakuwa juu ya kila mmoja
"itamuathiri kila mmoja" au "tukio la siku hiyo litamuathiri kila mmoja"
# katika uso wa dunia nzima
Tafsiri mbadala: "katika eneo la dunia nzima" au "juu ya dunia nzima"