sw_tn/luk/21/34.md

959 B

ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa

Tafsiri mbadala: "ili msije mkawa mmetingwa na"

ufisadi

"tamaa isiyoweza kuzuiwa" au " kujiweka kwenye kutamani na kutumia vitu ambavyo vinakufanya ujisikie vizuri." Tafsiri mbadala: "Anasa nyingi."

mahangaiko ya maisha haya

"kujitaabisha au kujihangaisha sana kuhusu maisha haya"

kwa sababu siku ile itawajia ghafula

Wengine wangependa kuongeza habari elekezi: "Kwamba kama hamtakuwa waangalifu ile siku itawajia ghafula." Ujio wa siku hiyo utaonekana kuwa wa ghafula na wakutotarajiwa kwa wale ambao hawako na hawaisubiri.

ile siku

Tafsiri mbadala: "siku ambayo Mwana wa Adamu atakuja"

ghafula kama mtego

Tafsiri mbadala: "wakati ambapo hamuitarajii, kama mtego unapofunga ghafula kwa mnyama"

itakuwa juu ya kila mmoja

"itamuathiri kila mmoja" au "tukio la siku hiyo litamuathiri kila mmoja"

katika uso wa dunia nzima

Tafsiri mbadala: "katika eneo la dunia nzima" au "juu ya dunia nzima"