# ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa Tafsiri mbadala: "ili msije mkawa mmetingwa na" # ufisadi "tamaa isiyoweza kuzuiwa" au " kujiweka kwenye kutamani na kutumia vitu ambavyo vinakufanya ujisikie vizuri." Tafsiri mbadala: "Anasa nyingi." # mahangaiko ya maisha haya "kujitaabisha au kujihangaisha sana kuhusu maisha haya" # kwa sababu siku ile itawajia ghafula Wengine wangependa kuongeza habari elekezi: "Kwamba kama hamtakuwa waangalifu ile siku itawajia ghafula." Ujio wa siku hiyo utaonekana kuwa wa ghafula na wakutotarajiwa kwa wale ambao hawako na hawaisubiri. # ile siku Tafsiri mbadala: "siku ambayo Mwana wa Adamu atakuja" # ghafula kama mtego Tafsiri mbadala: "wakati ambapo hamuitarajii, kama mtego unapofunga ghafula kwa mnyama" # itakuwa juu ya kila mmoja "itamuathiri kila mmoja" au "tukio la siku hiyo litamuathiri kila mmoja" # katika uso wa dunia nzima Tafsiri mbadala: "katika eneo la dunia nzima" au "juu ya dunia nzima"