sw_tn/luk/20/17.md

36 lines
1.2 KiB
Markdown

# Maelezo yanayounganisha
Yesu anaendelea kuwafundisha makutano
# Yesu akawaangalia
"Lakini yesu akawatazama" au "Lakini Yesu akawaangalia moja kwa moja." Alifanya hivi ili wamuelewe alichokuwa anakisema.
# Andiko hili lina maana gani?
"Andiko hili linaelezea nini?" Yesu alitumia maswali kuwauliza makutano. "Mnatakiwa kuwa na uwezo kuelewa aandiko hili"
# Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe la msingi
Fumbo hili ni unabii toka kitabu cha Zaburi kuhusu namna watu watakavyomkataa Masiha.
# Jiwe walilolikataa
"Jiwe walilolikataa waashi wakisema halikuwa zuri kwa ajili ya ujenzi." Kipindi hicho watu walijenga kuta za nyumba na majengo mengine kwa kutumia mawe.
# Limekuwa jiwe la msingi
Hili lilikuwa jiawe la muhimu kwa kufanya jengo liwe imara. "Limekuwa jiwe la Msingi" au "limekuwa jiwe la Muhimu"
# Kila atakayeanguka kwenye jiwe hilo.
"Yeyote atakayeanguka kwenye jiwe hilo". Fumbo hili ni unabii kuhusu kitakachotokea kwa wote watakaomkataa Mesia.
# Atavunjika vipande vipande
"Atavunjika vipande vipande." Haya ni matokeo ya kuanguka kwenye jiwe.
# Lakini kwa yeyote ambaye litamwangukia
"Lakini kwa yeyote ambaye jiwe litamwangukia." Fumbo hili linaonyesha unabii kuhusu Mesia atakapowahukumu waliomkataa.