sw_tn/luk/20/17.md

1.2 KiB

Maelezo yanayounganisha

Yesu anaendelea kuwafundisha makutano

Yesu akawaangalia

"Lakini yesu akawatazama" au "Lakini Yesu akawaangalia moja kwa moja." Alifanya hivi ili wamuelewe alichokuwa anakisema.

Andiko hili lina maana gani?

"Andiko hili linaelezea nini?" Yesu alitumia maswali kuwauliza makutano. "Mnatakiwa kuwa na uwezo kuelewa aandiko hili"

Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe la msingi

Fumbo hili ni unabii toka kitabu cha Zaburi kuhusu namna watu watakavyomkataa Masiha.

Jiwe walilolikataa

"Jiwe walilolikataa waashi wakisema halikuwa zuri kwa ajili ya ujenzi." Kipindi hicho watu walijenga kuta za nyumba na majengo mengine kwa kutumia mawe.

Limekuwa jiwe la msingi

Hili lilikuwa jiawe la muhimu kwa kufanya jengo liwe imara. "Limekuwa jiwe la Msingi" au "limekuwa jiwe la Muhimu"

Kila atakayeanguka kwenye jiwe hilo.

"Yeyote atakayeanguka kwenye jiwe hilo". Fumbo hili ni unabii kuhusu kitakachotokea kwa wote watakaomkataa Mesia.

Atavunjika vipande vipande

"Atavunjika vipande vipande." Haya ni matokeo ya kuanguka kwenye jiwe.

Lakini kwa yeyote ambaye litamwangukia

"Lakini kwa yeyote ambaye jiwe litamwangukia." Fumbo hili linaonyesha unabii kuhusu Mesia atakapowahukumu waliomkataa.