# Maelezo yanayounganisha Yesu anaendelea kuwafundisha makutano # Yesu akawaangalia "Lakini yesu akawatazama" au "Lakini Yesu akawaangalia moja kwa moja." Alifanya hivi ili wamuelewe alichokuwa anakisema. # Andiko hili lina maana gani? "Andiko hili linaelezea nini?" Yesu alitumia maswali kuwauliza makutano. "Mnatakiwa kuwa na uwezo kuelewa aandiko hili" # Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe la msingi Fumbo hili ni unabii toka kitabu cha Zaburi kuhusu namna watu watakavyomkataa Masiha. # Jiwe walilolikataa "Jiwe walilolikataa waashi wakisema halikuwa zuri kwa ajili ya ujenzi." Kipindi hicho watu walijenga kuta za nyumba na majengo mengine kwa kutumia mawe. # Limekuwa jiwe la msingi Hili lilikuwa jiawe la muhimu kwa kufanya jengo liwe imara. "Limekuwa jiwe la Msingi" au "limekuwa jiwe la Muhimu" # Kila atakayeanguka kwenye jiwe hilo. "Yeyote atakayeanguka kwenye jiwe hilo". Fumbo hili ni unabii kuhusu kitakachotokea kwa wote watakaomkataa Mesia. # Atavunjika vipande vipande "Atavunjika vipande vipande." Haya ni matokeo ya kuanguka kwenye jiwe. # Lakini kwa yeyote ambaye litamwangukia "Lakini kwa yeyote ambaye jiwe litamwangukia." Fumbo hili linaonyesha unabii kuhusu Mesia atakapowahukumu waliomkataa.