sw_tn/luk/12/49.md

24 lines
1.0 KiB
Markdown

# Kauli inayounganisha
Yesu aliendelea kufundisha wanafunzi wake
# Nimekuja kuwasha moto duniani
"Nimekuja kutupa moto duniani" au "Nimekuja kuwasha moto duniani" . Inawsza kuwa na maama zifuatazo: 1) Yesu alikuja kuwahukumu watu 2) Yesu alikuja kuwatakasa wanaomuamini 3) Yesu alikuja kusababisha kugawanyika kwa watu.
# natamani iwe imekwisha kuwaka
Kuna msisitizo wa njisi alivyotaka hayo yatokee. " Natamani sana kuwa imeshawaka" au "Ni jinsi gani ninavyotamani iwe imeshaanza"
# Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa kwayo
"Ubatizo" ina maanisha aina ya mateso ambayo Yesu atapata. Kama maji yamfinikavyo mtu wakati wa ubatizo, mateso yatamkabili na kumpata Yesu. " Ni lazima nipitie mateso mabaya" au "Nitapitia katika mateso makubwa kama vile mtu anavyofunikwa na maji wakati wa ubatizo"
# Lakini
Neno "Lakini" linatumika kuonyesha kuwa hatawasha moto duniani mpaka kwanza apitie hayo mateso"
# nina huzuni hadi ikamilike
Mshangao inasisitiza jinsi alivyo na huzuni. "Nina huzuni sana na itaendelea kuwepo hadi nimalize ubatizo huu wa mateso"