sw_tn/luk/12/49.md

1.0 KiB

Kauli inayounganisha

Yesu aliendelea kufundisha wanafunzi wake

Nimekuja kuwasha moto duniani

"Nimekuja kutupa moto duniani" au "Nimekuja kuwasha moto duniani" . Inawsza kuwa na maama zifuatazo: 1) Yesu alikuja kuwahukumu watu 2) Yesu alikuja kuwatakasa wanaomuamini 3) Yesu alikuja kusababisha kugawanyika kwa watu.

natamani iwe imekwisha kuwaka

Kuna msisitizo wa njisi alivyotaka hayo yatokee. " Natamani sana kuwa imeshawaka" au "Ni jinsi gani ninavyotamani iwe imeshaanza"

Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa kwayo

"Ubatizo" ina maanisha aina ya mateso ambayo Yesu atapata. Kama maji yamfinikavyo mtu wakati wa ubatizo, mateso yatamkabili na kumpata Yesu. " Ni lazima nipitie mateso mabaya" au "Nitapitia katika mateso makubwa kama vile mtu anavyofunikwa na maji wakati wa ubatizo"

Lakini

Neno "Lakini" linatumika kuonyesha kuwa hatawasha moto duniani mpaka kwanza apitie hayo mateso"

nina huzuni hadi ikamilike

Mshangao inasisitiza jinsi alivyo na huzuni. "Nina huzuni sana na itaendelea kuwepo hadi nimalize ubatizo huu wa mateso"