# Kauli inayounganisha Yesu aliendelea kufundisha wanafunzi wake # Nimekuja kuwasha moto duniani "Nimekuja kutupa moto duniani" au "Nimekuja kuwasha moto duniani" . Inawsza kuwa na maama zifuatazo: 1) Yesu alikuja kuwahukumu watu 2) Yesu alikuja kuwatakasa wanaomuamini 3) Yesu alikuja kusababisha kugawanyika kwa watu. # natamani iwe imekwisha kuwaka Kuna msisitizo wa njisi alivyotaka hayo yatokee. " Natamani sana kuwa imeshawaka" au "Ni jinsi gani ninavyotamani iwe imeshaanza" # Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa kwayo "Ubatizo" ina maanisha aina ya mateso ambayo Yesu atapata. Kama maji yamfinikavyo mtu wakati wa ubatizo, mateso yatamkabili na kumpata Yesu. " Ni lazima nipitie mateso mabaya" au "Nitapitia katika mateso makubwa kama vile mtu anavyofunikwa na maji wakati wa ubatizo" # Lakini Neno "Lakini" linatumika kuonyesha kuwa hatawasha moto duniani mpaka kwanza apitie hayo mateso" # nina huzuni hadi ikamilike Mshangao inasisitiza jinsi alivyo na huzuni. "Nina huzuni sana na itaendelea kuwepo hadi nimalize ubatizo huu wa mateso"