sw_tn/luk/11/18.md

28 lines
1.2 KiB
Markdown

# kama shetani takuwa amegawanyika
"Shetani" hapa inawakilisha wale mapepo waliojiunga na Shetani kumuasi Mungu. "Kama shetani na washirika wa ufalme wake wanapigan a wao kwa wao"
# ufalme wake utasimamaje?
Yesu alitumia maswali kufundisha watu. "Ufalme wa Shetani hautadumu" au "Ufalme wa shetani utaanguka na kusambaratika"
# Kwasababu mwasema natoa mapepo kwa Belzebuli
Kwa sababu mwasema ni kwa nguvu ya Belzebuli nawafanya mapepo kuwaacha watu . sehemu iliyofuata ya majibu yake inaweza kutamkwa kirahisi: "hii inamaana Shetani amegawachika juu yake"
# Je wenzenu wanatoa mapepo kwa njia gani?
"ni kwa nguvu ya nani wenzenu wanawaamurisha mapepo kuwaacha watu. " Yesu alitumia swali kufundisha watu.Swali la Yesu inaweza kurahisishwa, "basi ni lazima tukubaliane kuwa wenzenu pia hutumia nguvu ya Beelzebuli kuondoa mapepo". "Lakini tunajua kuwa hiyo si kweli".
# wao watawahukumu ninyi
wenzenu wanao watoa mapepo kwa nguvu ya Mungu watawahukumu ninyi kwa kusema kuwa mimi natoa mapepo kwa nguvu ya Beelzebuli.
# kwa kidole cha Mungu
"Kidole cha Mungu" inamaanisha ni Nguvu ya Mungu
# Basi ufalme wa Mungu umewajia
"Hii inaonyesha kuwa ufalme wa Mungu umekuja kwenu"