# kama shetani takuwa amegawanyika "Shetani" hapa inawakilisha wale mapepo waliojiunga na Shetani kumuasi Mungu. "Kama shetani na washirika wa ufalme wake wanapigan a wao kwa wao" # ufalme wake utasimamaje? Yesu alitumia maswali kufundisha watu. "Ufalme wa Shetani hautadumu" au "Ufalme wa shetani utaanguka na kusambaratika" # Kwasababu mwasema natoa mapepo kwa Belzebuli Kwa sababu mwasema ni kwa nguvu ya Belzebuli nawafanya mapepo kuwaacha watu . sehemu iliyofuata ya majibu yake inaweza kutamkwa kirahisi: "hii inamaana Shetani amegawachika juu yake" # Je wenzenu wanatoa mapepo kwa njia gani? "ni kwa nguvu ya nani wenzenu wanawaamurisha mapepo kuwaacha watu. " Yesu alitumia swali kufundisha watu.Swali la Yesu inaweza kurahisishwa, "basi ni lazima tukubaliane kuwa wenzenu pia hutumia nguvu ya Beelzebuli kuondoa mapepo". "Lakini tunajua kuwa hiyo si kweli". # wao watawahukumu ninyi wenzenu wanao watoa mapepo kwa nguvu ya Mungu watawahukumu ninyi kwa kusema kuwa mimi natoa mapepo kwa nguvu ya Beelzebuli. # kwa kidole cha Mungu "Kidole cha Mungu" inamaanisha ni Nguvu ya Mungu # Basi ufalme wa Mungu umewajia "Hii inaonyesha kuwa ufalme wa Mungu umekuja kwenu"