sw_tn/luk/04/25.md

32 lines
1.2 KiB
Markdown

# Sentensi kwa Ujumla
Yesu anawakumbusha watu, wanaomsikiliza kwenye sinagogi, kuhusu Eliya na Elisha waliokuwa manabii ambao waliwafahamu.
# Lakini nawaambia ukweli
"Nawaambia ukweli kabisa." Kauli hii ilitumika kusisitiza umhimu, ukweli na usahihi wa kauli zinazofuata.
# wajane
mjane ni mwanamke aliyefiwa na mume wake.
# wakati wa Eliya
Watu wale aliokuwa anawahutubia walijua kwamba Eliya alikuwa mmoja wa manabii wa Mungu. Kama wasomaji wako hawatajua hilo, unaweza ukafanya taarifa zisizowazi kuwa wazi kma UDB. AT: "Eliya alipokuwa anatoa unabii Israel"
# wakati wingu lilipofungwa
Hii ni sitiari. Anga limefananishwa na dari iliyofungwa, na hivyo hakuna mvua itakayonyysha toka huko. NI: "ambapo hakuna mvua inashuka chini kutoka angani" au "wakati ilikuwa hakuna mvua kabisa"
# njaa kubwa
"tatizo kubwa la kupungua chakula." Njaa ni kipindi kirefu ambapo hakuna uzalishaji wa mazo ya kutosha chakula kwa watu.
# mpaka Sarepta ... kwa mjane anayeishi huko
Watu walioishi Sarepta walikuwa Wamataifa, siyo Wayahudi. Watu wanaomsikiliza Yesu wangeelewa kwamaba watu wa Sarepta walikuwa Wamataifa. Mjane mmataifa anaishi Sarepta.
# Naamani Msiria
Msiria ni mtu kutoka nchi ya Siria. Watu wa Siria ni siyo Wayahudi. NI: "Mmataifa Naamani kutoka Siria"