sw_tn/luk/04/25.md

1.2 KiB

Sentensi kwa Ujumla

Yesu anawakumbusha watu, wanaomsikiliza kwenye sinagogi, kuhusu Eliya na Elisha waliokuwa manabii ambao waliwafahamu.

Lakini nawaambia ukweli

"Nawaambia ukweli kabisa." Kauli hii ilitumika kusisitiza umhimu, ukweli na usahihi wa kauli zinazofuata.

wajane

mjane ni mwanamke aliyefiwa na mume wake.

wakati wa Eliya

Watu wale aliokuwa anawahutubia walijua kwamba Eliya alikuwa mmoja wa manabii wa Mungu. Kama wasomaji wako hawatajua hilo, unaweza ukafanya taarifa zisizowazi kuwa wazi kma UDB. AT: "Eliya alipokuwa anatoa unabii Israel"

wakati wingu lilipofungwa

Hii ni sitiari. Anga limefananishwa na dari iliyofungwa, na hivyo hakuna mvua itakayonyysha toka huko. NI: "ambapo hakuna mvua inashuka chini kutoka angani" au "wakati ilikuwa hakuna mvua kabisa"

njaa kubwa

"tatizo kubwa la kupungua chakula." Njaa ni kipindi kirefu ambapo hakuna uzalishaji wa mazo ya kutosha chakula kwa watu.

mpaka Sarepta ... kwa mjane anayeishi huko

Watu walioishi Sarepta walikuwa Wamataifa, siyo Wayahudi. Watu wanaomsikiliza Yesu wangeelewa kwamaba watu wa Sarepta walikuwa Wamataifa. Mjane mmataifa anaishi Sarepta.

Naamani Msiria

Msiria ni mtu kutoka nchi ya Siria. Watu wa Siria ni siyo Wayahudi. NI: "Mmataifa Naamani kutoka Siria"