sw_tn/luk/02/25.md

28 lines
959 B
Markdown

# Kauli Unganishi:
Wakati Mariamu na Yusufu wako hekaluni, waliwaona watu wawili: Simeoni, ambaye alimsifu Mungu na kutoa unabii kuhusu mtoto, na nabii mke Ana.
# Tazama
Neno "tazama" linatuashiria mtu mpya katika simulizi. Lugha yako inaweza ikawa na njia ya kutenda hivi.
# alikuwa mwenye haki na mcha Mungu
Kauli za nadharia hizi zinaweza kudhihirishwa kama matendo. NI: "alifanya kilichokuwa kinamridhisha Mungu na alitii sheria za Mungu."
# mfariji wa Israeli
Hili ni jina jingine la "Masihi" au "Kristo." NI: "ndiye ambaye atafariji Israeli."
# Roho Mtakatifu alikuwa juu yake
"Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye." Mungu alikuwa pamoja naye katika njia maalumu na alimpa hekima na maelekezo katika maisha yake.
# ikafunuliwa kwake na Roho Mtakatifu
Hii inaweza kusemwa katika mtindo tendea. NI: "Roho Mtakatifu akamwonesha" au "Roho Mtakatifu akamwambia."
# asingalikufa kabla hajamwona Kristo Bwana
"angelimwona Masihi Bwana kabla hajafa"