sw_tn/luk/02/25.md

959 B

Kauli Unganishi:

Wakati Mariamu na Yusufu wako hekaluni, waliwaona watu wawili: Simeoni, ambaye alimsifu Mungu na kutoa unabii kuhusu mtoto, na nabii mke Ana.

Tazama

Neno "tazama" linatuashiria mtu mpya katika simulizi. Lugha yako inaweza ikawa na njia ya kutenda hivi.

alikuwa mwenye haki na mcha Mungu

Kauli za nadharia hizi zinaweza kudhihirishwa kama matendo. NI: "alifanya kilichokuwa kinamridhisha Mungu na alitii sheria za Mungu."

mfariji wa Israeli

Hili ni jina jingine la "Masihi" au "Kristo." NI: "ndiye ambaye atafariji Israeli."

Roho Mtakatifu alikuwa juu yake

"Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye." Mungu alikuwa pamoja naye katika njia maalumu na alimpa hekima na maelekezo katika maisha yake.

ikafunuliwa kwake na Roho Mtakatifu

Hii inaweza kusemwa katika mtindo tendea. NI: "Roho Mtakatifu akamwonesha" au "Roho Mtakatifu akamwambia."

asingalikufa kabla hajamwona Kristo Bwana

"angelimwona Masihi Bwana kabla hajafa"