# Kauli Unganishi: Wakati Mariamu na Yusufu wako hekaluni, waliwaona watu wawili: Simeoni, ambaye alimsifu Mungu na kutoa unabii kuhusu mtoto, na nabii mke Ana. # Tazama Neno "tazama" linatuashiria mtu mpya katika simulizi. Lugha yako inaweza ikawa na njia ya kutenda hivi. # alikuwa mwenye haki na mcha Mungu Kauli za nadharia hizi zinaweza kudhihirishwa kama matendo. NI: "alifanya kilichokuwa kinamridhisha Mungu na alitii sheria za Mungu." # mfariji wa Israeli Hili ni jina jingine la "Masihi" au "Kristo." NI: "ndiye ambaye atafariji Israeli." # Roho Mtakatifu alikuwa juu yake "Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye." Mungu alikuwa pamoja naye katika njia maalumu na alimpa hekima na maelekezo katika maisha yake. # ikafunuliwa kwake na Roho Mtakatifu Hii inaweza kusemwa katika mtindo tendea. NI: "Roho Mtakatifu akamwonesha" au "Roho Mtakatifu akamwambia." # asingalikufa kabla hajamwona Kristo Bwana "angelimwona Masihi Bwana kabla hajafa"