sw_tn/luk/02/01.md

1.4 KiB

Maelezo kwa ujumla

Hii inatoa maelezo ya nyuma kuonesha kwanini Mariamu na Yusufu wanatakiwa kuondoka kwaajili ya kuzaliwa kwa Yesu.

Sasa

Neno hili ni alama ya kuanza kwa sehemu mpya ya simulizi.

ikaja ikawa kwamba

Kauli hii ilitumika kuonesha kwamba huu ni mwanzo wa wajibu. Kama lugha yako inayo njia ya kuonesha kuanza kwa kuwajibika, unaweza ukatumia hiyo. Baadhi ya tafsiri haziweki kauli hii.

Kaisari Agusto

"Mfalme Agusto" au "Mtawala Agusto." Agusto alikuwa mtawala wa kwanza wa dola ya Rumi.

alitoa agizo likielekeza

Amri hii huenda ilinabebwa na wajumbe kupitia katika dola. NI: "wajumbe waliotumwa maelekezo ya amri"

kwamba ichukuliwe sensa ya watu wote wanaoishi katika ulimwengu

Hii inaweza kusemwa katika mtindo wa kutendea. NI: "kwamba waorodheshe watu wote wanaoishi katika ulimwengu wa kirumi" au "wahesabu watu wote katika ulimwengu wa kirumi na waandike majina yao."

ulimwengu

eneo la dunia lililotawaliwa na serikali ya Rumi au "nchi zilizoongozwa na dola ya Kirumi"

Krenio

Krenio aliteuliwa kuwa mtawala wa Siria/Shamu

kila mmoja alikwenda

"kila mmoja aliondoka" au "kila mmoja alikuwa anakwenda"

mji wa kwao

Inaweza ikasaidia kusema kwamba "ya kwake" hairejei kwenye mji ambao alikuwa akiishi. NI: "ni mji ambao wahenga wake waliishi."

kuandikishwa kwaajili ya sensa

"kuwa na majina yameandikwa kwenye orodha" au "kuwekwa kwenye idadi kiofisi"