sw_tn/luk/02/01.md

44 lines
1.4 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Maelezo kwa ujumla
Hii inatoa maelezo ya nyuma kuonesha kwanini Mariamu na Yusufu wanatakiwa kuondoka kwaajili ya kuzaliwa kwa Yesu.
# Sasa
Neno hili ni alama ya kuanza kwa sehemu mpya ya simulizi.
# ikaja ikawa kwamba
Kauli hii ilitumika kuonesha kwamba huu ni mwanzo wa wajibu. Kama lugha yako inayo njia ya kuonesha kuanza kwa kuwajibika, unaweza ukatumia hiyo. Baadhi ya tafsiri haziweki kauli hii.
# Kaisari Agusto
"Mfalme Agusto" au "Mtawala Agusto." Agusto alikuwa mtawala wa kwanza wa dola ya Rumi.
# alitoa agizo likielekeza
Amri hii huenda ilinabebwa na wajumbe kupitia katika dola. NI: "wajumbe waliotumwa maelekezo ya amri"
# kwamba ichukuliwe sensa ya watu wote wanaoishi katika ulimwengu
Hii inaweza kusemwa katika mtindo wa kutendea. NI: "kwamba waorodheshe watu wote wanaoishi katika ulimwengu wa kirumi" au "wahesabu watu wote katika ulimwengu wa kirumi na waandike majina yao."
# ulimwengu
eneo la dunia lililotawaliwa na serikali ya Rumi au "nchi zilizoongozwa na dola ya Kirumi"
# Krenio
Krenio aliteuliwa kuwa mtawala wa Siria/Shamu
# kila mmoja alikwenda
"kila mmoja aliondoka" au "kila mmoja alikuwa anakwenda"
# mji wa kwao
Inaweza ikasaidia kusema kwamba "ya kwake" hairejei kwenye mji ambao alikuwa akiishi. NI: "ni mji ambao wahenga wake waliishi."
# kuandikishwa kwaajili ya sensa
"kuwa na majina yameandikwa kwenye orodha" au "kuwekwa kwenye idadi kiofisi"