sw_tn/luk/01/64.md

1.3 KiB

kinywa chake kilifunguliwa ... ulimi wake uliwekwa huru

Hizi kauli mbili ni maneno picha ambayo pamoja yanasisitiza kwamba Zakaria aliweza kuzungumza ghafla.

kinywa chake kilifunguliwa na ulimi wake uliwekwa huru

Kauli hizi zinaweza pia kusemwa katika mtindo wa kutenda. NI: Mungu akafungua kinywa chake na kuuweka huru ulimi."

Hofu ikawajia wote ambao waliishi karibu nao

"Wote walioishi karibu na Zakaria na Elizabethi walikuwa na hofu." Walikuwa wamepigwa butwaa kwa njia ya Mungu ya miujiza kumrejeshea Zakaria uwezo wa kuzungumza. NI: "Kila mmoja aliyeishi karibu nao walikuwa katika hofu ya Mungu."

wote ambao waliishi

Hii hairejei tu kwa wale majirani wa karibu lakini kwa kila mmoja ambaye aliishi eneo hilo.

wote waliowasikia wao

Neno "wao" hapa linarejea kwenye mambo yaliokwisha tokea.

wote waliosikia

Hii inarejea kwenye kundi kubwa la watu walioishi Uyahudi yote.

kusema

"kuuliza"

Mtoto huyu atakuja kuwa kuwa nani?

"Aina gani ya ukuu ambao atakuwa nao mtoto huyu akikua?" Hii pia inawezeakana kwamba swali hili lilikuwa linamaanisha kuwa ni kauli ya kuwashangaza kwa kile walichisikia kuhusu mtoto. NI: "Mtoto huyu atakuwa mkuu wa namna gani!"

mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye

Kauli hii "mkono wa Bwana" inarejea nguvu za Mungu. "Nguvu za Mungu zilikuwa pamoja naye" au "Mungu alikuwa anafanya kazi ndani yake kwa nguvu."