sw_tn/luk/01/64.md

36 lines
1.3 KiB
Markdown
Raw Permalink Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# kinywa chake kilifunguliwa ... ulimi wake uliwekwa huru
Hizi kauli mbili ni maneno picha ambayo pamoja yanasisitiza kwamba Zakaria aliweza kuzungumza ghafla.
# kinywa chake kilifunguliwa na ulimi wake uliwekwa huru
Kauli hizi zinaweza pia kusemwa katika mtindo wa kutenda. NI: Mungu akafungua kinywa chake na kuuweka huru ulimi."
# Hofu ikawajia wote ambao waliishi karibu nao
"Wote walioishi karibu na Zakaria na Elizabethi walikuwa na hofu." Walikuwa wamepigwa butwaa kwa njia ya Mungu ya miujiza kumrejeshea Zakaria uwezo wa kuzungumza. NI: "Kila mmoja aliyeishi karibu nao walikuwa katika hofu ya Mungu."
# wote ambao waliishi
Hii hairejei tu kwa wale majirani wa karibu lakini kwa kila mmoja ambaye aliishi eneo hilo.
# wote waliowasikia wao
Neno "wao" hapa linarejea kwenye mambo yaliokwisha tokea.
# wote waliosikia
Hii inarejea kwenye kundi kubwa la watu walioishi Uyahudi yote.
# kusema
"kuuliza"
# Mtoto huyu atakuja kuwa kuwa nani?
"Aina gani ya ukuu ambao atakuwa nao mtoto huyu akikua?" Hii pia inawezeakana kwamba swali hili lilikuwa linamaanisha kuwa ni kauli ya kuwashangaza kwa kile walichisikia kuhusu mtoto. NI: "Mtoto huyu atakuwa mkuu wa namna gani!"
# mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye
Kauli hii "mkono wa Bwana" inarejea nguvu za Mungu. "Nguvu za Mungu zilikuwa pamoja naye" au "Mungu alikuwa anafanya kazi ndani yake kwa nguvu."