sw_tn/luk/01/11.md

1.1 KiB

Sentensi Unganishi:

Wakati Zakaria anafanya wajibu wake hekaluni, malaika anakuja kutoka kwa Mungu kumpa ujumbe.

Sasa

Neno hili linazingatia mwanzo wa kitendo katika historia,

alimtokea

"ghafla alikuja kwake" au "ghafla alikuwa pale pamoja na Zakaria." Hii inaweka wazi kwamba malaika alikuwa pamoja na Zakaria, na siyo tu maono.

Zakaria ... alikuwa katekewa ... woga ukamwangukia

Hizi kauli mbili zinamaana ileile, na zinasisitiza jinsi Zakaria alivyokuwa na hofu.

Zakaria alipomuona

"Zakaria alipomwona malaika" Chanzo cha hofu kilikuwa kushituliwa na ile asili ya malaika. Zakaria hakufanya kitu chochote kibaya.

Hofu ikaja juu yake

Hofu ni kitu kinachofafanuliwa kama kwamba shambulio au Zakaria alizidiwa nguvu.

Usiogope

"usiendelee kuniogopa mimi" au "Wewe hutakiwi kuniogopa mimi"

maombi yako yamesikiwa

"Mungu amesikia ambacho uliomba." Kinachofuata kinadokeza na kingeliongezwa: "ataruhusu hiyo." Mungu hakukomea kusikia tu alichoomba Zakaria; pia alikuwa anaelekea kutenda.

utazaa mwana

"mwana wa kiume kwaajili yako" au "kuzaa mtoto wako wa kiume"